Tuesday, 22 May 2018

KARIBU



 AMANI YA YESU IWE NANYI
tunawasalimu kwa jina la Bwana Yesu Kristo aliye
Mzaliwa wa Kwanza wa Viumbe Vyote
aliyekubali kuacha enzi na mamlaka huko mbinguni kwa ajili yetu.

TUNAOMBA RADHI KWA WASOMAJI WETU
kwa ukimya wa kipindi kirefu,
hii ni kutaokana na sababu ambazo hata hivyo
YESU AMEZIONDOA na sasa tunarudi kwa UWEZA WAKE YESU

aidha tunapenda kuwashukuru wale ambao
kwa kipindi kirefu wamekuwa bado wakifuatilia
na kuuliza maswali kupitia email, hata wale ambao walifuatilia
humu kwa namna ingine.

YESU yu hai milele na bado anafanya kazi kati ya wale
wampendao. karibu tuendelee kujifunza siri zake
maana YESU hakuja kutafuta WAKRISTO BALI
alikuja kutafuta WANAFUNZI WAKE ( Mathayo 28:19-20)

KARIBUNI TUFUNDISHANE NENO LA KRISTO.





Hii ni blog yenye kubeba Maneno ya Mungu wa Israel na mwanae YESU Kristo wa Nazareti na Nguvu ya Roho Mtakatifu.
Ni blog isiyo fungamana na dhehebu lolote, wala utaratibu wa kanuni za dhehebu lolote, BALI imefungwa na Neno la Uhai la Mungu aliye hai Mungu wa Yesu Kristo.
Iko kwa ajili ya kulifanya kanisa la Kristo ambalo ndio mwili wa Kristo na bibi harusi wa Kristo, kujifunza juu ya njia na Maagizo ya Mungu wa Israel, na namna ya kuzifuata njia hizi. Ili mwisho wa kila Kanisa lipate kupewa nafasi na BWANA ya kumkaribia kati yao wasimamao karibu nae.

Karibu tuungane na mwalimu DORIS BARNABAS K. KULLWA (MRS) na  DANIEL EMANUEL KULLWA (MR) kujifunza juu ya njia na maagizo ya BWANA Wetu Mungu wa Majeshi, Yehova, Yahu, Niko ambaye Niko, Alfa na Omega, Mungu Mwenyezi, Mfalme wa Wafalme na Baba wa milele.